Wafanyakazi wa Benki ya CBA washerehekea pasaka na watoto yatima
Benki
ya Commercial Bank of Africa (CBA) leo imetoa msaada wa vitu mbalimbali
kwa watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo cha Msimbazi kilichopo Ilala
jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wafanyakazi hao walishiriki kulea
na kucheza na watoto hao ikiwa ni njia ya kuwaonyesha upendo.
Akizungumza
kituoni hapo Meneja wa benki hiyo wa tawi la Nyerere ,Nuru
Mwangulangu,ambaye aliongoza wafanyakazi wenzake waliofika kituoni hapo
alisema wamefanya hivyo kama sehemu ya utaratibu wao wa kuchangia
makundi yenye mahitaji maalumu kwenye jamii hususani watoto ambao ndio
tunaamini wanapaswa kuandaliwa vizuri na kupata mahitaji muhimu na haki
wanazostahili kwa kuwa ndio taifa la kesho.
“CBA
leo tumekuja kuwaona vijana, kufurahi nao,na kuwapatia zawadi ili
kuwawezesha kufurahia sikukuu ya Pasaka kama watoto wengine waliopo
majumbani.watoto kama hawa wanahitaji upendo,faraja na kupatiwa misaada
mbalimbali ya kuwawezesha kujisikia kuwa nao ni sehemu ya jamii na
kusaidia jamii ni sehemu ya sera yetu ndio maana tumekuwa tukisaidia
jamii katika Nyanja mbalimbali hususani elimu na afya”.Alisema
Mwangulangu.
Pia
alisema kufika kwao wameweza kuangalia mazingira, kufahamu changamoto
zinazowakabili walezi wa kituo hicho na kuona wapi benki inaweza
kusaidia katika siku za usoni na aliwataka wadau mbalimbali kujitokeza
kusaidia kutoa msaada na kutumia muda wao kusaidia makundi mbalimbali
yenye mahitaji kwenye jamii.
Kwa
upande wake Msimamizi Mkuu wa kituo hicho,Sista Ana
Marandu,aliwashukuru wafanyanyakazi wa benki hiyo kwa kutoa msaada wa
chakula ,nguo,kuwafungia watoto michezo ya burudani na kutumia muda wao
kucheza nao. “Tunatoa shukrani kwa upendo mkubwa mlioonyesha siku hii ya
leo na tunawaomba siku zote mtupe ushirikiano kama huu”.Alisema Sista
Marandu.
Wafanyakazi wa Benki ya CBA washerehekea pasaka na watoto yatima
Reviewed by crispaseve
on
09:09
Rating:
Post a Comment