WAZIRI MEMBE ATOA RAI KWA VIONGOZI WA DINI ZOTE KUHIMIZA VIJANA WAIPENDE DINI KUDUMISHA AMANI NCHINI
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe
akionyesha tuzo yake mbele ya umati wa watu (hawapo
pichani),aliyotunukiwa kwa mchango wake mkubwa kwa shughuli mbalimbali
za kijamii,katika tamasha la pasaka.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ambaye
alikuwa mgeni rasmi akiongea katika tamasha la 15 la Pasaka
lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5,
2015. Pembeni ni Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ametoa
rai kwa viongozi wa dini zote pamoja serikali kuhimiza vijana waipende
dini ili kudumisha amani, utulivu na uadilifu.Mhe Membe amesema hayo
wakati akihubutubi maelfu ya watu waliohudhuria Tamasha la 15 la Pasaka,
lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5,
2015.
Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly akisoma hotuba
amempongeza Mhe Bernard Membe kwa kujumuika na Watanzania katika
Tamasha la kumi na tano la Pasaka.Katika Tamasha hilo la Pasaka, Kampuni
ya Msama Promotions, ambao ndio waandaji wa Tamasha hilo, wamemtunuku
Mhe. Rais Jakaya Kikwete kwa mchango wake katika kukuza tasnia ya Sanaa
nchini.
Tuzo ya heshima ilitolewa kwa Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi.
Mhe
Bernard Membe alitunukiwa tuzo kwa mchango wake kwa shughuli za
kijamii.Tuzo zimetolewa kwa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwa
michango yao katika kutangaza Tamasha la Pasaka.
Viongozi
wa Serikali waliohudhuria Tamasha hilo ni pamoja na Mhe. Fenella
Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Angela
Kairuki, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na Mhe.
Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.Tamasha hilo lilihudhuriwa na
viongozi wa kidini wakiwemo, Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth
Gospel Assembly na Mchungaji Mwasota.
Tamasha
la Pasaka lilianzishwa rasmi mwaka 2000 na huwashirikisha Waimbaji wa
Nyimbo za Injili kutoka nchini na nje ya nchi ambapo mwaka huu
limewashirikisha waimbaji kutoka hapa nchini, Afrika Kusini, Uingereza na Zambia.
Mwanamuziki
wa Kimataifa wa nyimbo za Injili kutoka nchini Afrika Kusini,Rebecca
Malope akicheza na shabiki wake kwa staili ya pekee kabisa,huku uwanja
ukilipukwa na mayowe kila kona.
Mdau
wa muziki wa Injili Emmanuel Mbasha akipa kitu cha Selfie na rafiki
yake ndani ya uwanja wa Taifa wakati wa tamasha Pasaka lililofanyika
April 5 jijini Dar na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.
Kwaya
ya Kijitonyama wakiimba katika tamasha la 15 la Pasaka,
lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5,
2015.
Sehemu ya umati wa Watu waliohudhuria tamasha la 15 la
Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam,
Jumapili 5, 2015.
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na mkewe wakimkaribisha jukwaani Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe pichani kulia ni Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly.
WAZIRI MEMBE ATOA RAI KWA VIONGOZI WA DINI ZOTE KUHIMIZA VIJANA WAIPENDE DINI KUDUMISHA AMANI NCHINI
Reviewed by crispaseve
on
09:12
Rating:
Post a Comment