MAMA SALMA AWASILI NAIROBI KUHUDHURIA MKUTANO WA WAKE WA MARAIS WA AFRIKA KUHUSU KANSA YA MATITI,SHINGO YA KIZAZI NA TEZI DUME.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akipokea ua kutoka kwa binti Esther Wanjiru anayelelewa katika Kituo cha
watoto cha Mama Ngina huko Nairobi muda mfupi baada ya kuwasili kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya tarehe
19.7.2015. Mama Salma yupo nchini Kenya kuhudhuria Mkutano wa 9 wa wake
wa Marais wa Nchi za Afrika unaozungumzia masuala ya kansa Barani
Afrika.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akitia saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kutua kwenye Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta huko Narobi tarehe 19.7.2015.
Aliyesimama nyuma kulia ni Mheshimiwa Korere Sarah, Mbunge wa Jimbo la
Laikipya katika Mkoa wa Rift Valley aliyekuja kumpokea rasmi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiambatana na Mheshimiwa Korere Sarah wakipata mapumziko mafupi kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta kabla ya kuelekea
hotelini walikopangiwa.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya
Ndugu John Haule akisalimiana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati
alipowasili kwenye Hoteli ya Intercontinental iliyoko Nairobi tarehe
19.7.2015 kuhudhuria mkutano wa siku tatu wa wake wa Marais wa Afrika
utakaozungumzia magonjwa ya kansa ya shingo ya kizazi, matiti na tezi
dume.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akizungumza na Mke wa Rais wa Kenya Mama Margret Kenyatta wakati wa
tafrija ya kuwakaribisha kwenye mkutano wa 9 wa Wake wa Marais na Wakuu
wa Nchi za Afrika unaozungumzia masuala ya kansa ya matiti, shingo ya
kizazi na tezi dume. Tafrija hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya
Intercontinental jijini Nairobi tarehe 19.7.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akisalimiana na Madame Lordina Draman Mahama, Mke wa Rais wa Ghana
wakati wa tafrija ya kuwakaribisha iliyofanyika kwenye Hoteli ya
Intercontinental jijini Nairobi tarehe 19.7.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akifanya mazungumzo na Mke wa Rais wa Niger Dkt. Lalla Malika Issofou
Mahammadou wakati wa tafrija ya kuwakaribisha wajumbe wa mkutano wa 9 wa
wake wa Marais wa Africa wanaokutana Nairobi kuzungumzia kansa ya
matiti, kizazi na tezi dume.
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akifanya mazungumzo na Mke wa Rais wa Namibia Mheshimiwa Monica
Geingob wakati wa tafrija kwa wajumbe wa mkutanon wa 9 wa wake wa Marais
wa nchi za Afrika tarehe 19,7.2015. PICHA NA JOHN LUKUWI
MAMA SALMA AWASILI NAIROBI KUHUDHURIA MKUTANO WA WAKE WA MARAIS WA AFRIKA KUHUSU KANSA YA MATITI,SHINGO YA KIZAZI NA TEZI DUME.
Reviewed by crispaseve
on
05:34
Rating:
Post a Comment