Header AD

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI.


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  JESHI LA POLISI TANZANIA



“PRESS RELEASE” TAREHE 23.07.2015.

·    MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBARALI.

·        JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA POMBE KALI NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE KATIKA SHULE YA SEKONDARI MSHIKAMANO ILIYOPO KATIKA WILAYA YA MBARALI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GIDION MPUGI (20) MKAZI WA UHAMBULE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.618 CQH AINA YA MITSUBISHI FUSO ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA FRANK EVARISTO NYOTA (36) MKAZI WA UBARUKU.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 22.07.2015 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAJEN, KATA YA IGURUSI, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA NA UPELELEZI UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE VYA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO MVYA MOTO IKIWA NI PAMAOJA NA KUFUATA NA KUZINGATIA SHERIA, ALAMA NA MICHORO YA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


KATIKA TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA MAKUNGURU JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AGATHON SANGA (18) AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI AINA YA DOUBLE PUNCH KATONI 04, BOSS KATONI 02 NA CHARGER KATONO 01.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 22.07.2015 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO KATIKA MAENEO YA KABWE, KATA YA MAANGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.

KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LIMEKAMATA VIPODOZI MBALIMBALI VILIVYOPIGWA MARUFUKU NCHINI BAADA YA KUFANYA MSAKO KATIKA NYUMBA MOJA HUKO KATIKA MAENEO YA ITEZI, KATA YA ITEZI, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA  MKOA WA MBEYA.

KATIKA MSAKO HUO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 22.07.2017 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI, VIPODOZI AINA YA BUTA SOAP PIECE 50, EXTRA CLAIR PIECE 18 NA CAROLOGHT PIECE 12 VILIKAMATWA BAADA YA MTUHUMIWA KUWAONA POLISI NA KUKIMBIA NA KUVITELEKEZA VIPODOZI HIVYO. MSAKO MKALI UNAENDELEA KUMTAFUTA MTUHUMIWA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA UINGIZAJI/USAMBAZAJI NA UUZAJI WA POMBE KALI NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU NCHINI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

Imesainiwa:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI. TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI. Reviewed by crispaseve on 02:25 Rating: 5

No comments

Post AD