MTOTO MWENYE KIPAJI CHA AJABU KUTOKA MAREKANI ATUA NCHINI LEO, KUFANYA KONGAMANO LA WATOTO NA WAZAZI KESHO JIJINI DAR ES SALAAM
Na Mwandishi Wetu
MTOTO
mwenye kipawa cha ajabu katika kutoa ushauri wa kujijengea uwezo wa
kujiamini anayezidi kujipatia umaarufu mkubwa duniani, Lonnie Hudson
maarufu kama ‘King Nahh’(Pichani), ametua jijini Dar es Salaam , leo.
King
Nahh aliambatana na baba yake mzazi , Nyeeam Hudson ambapo wapo nchini
kwa mwaliko wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Wisdom Partners.
Kesho
mtoto huyo atafanya kongamano kubwa la watoto na wazazi katika
Ukumbi wa Urafiki ambapo nia na madhumuni ni kuamsha hisia za watu
ambao wamekata tamaa katika masuala mbalimbali na kukosa kujiamini
katika maamuzi.
“Najisikia
furaha kuja Tanzani. Ninaamini nina jukumu kubwa la kufanya hapa.
Hususani kwa watoto ambao bado hawaamini kuwa wanaweza kubadili hisia
zao, kujiamini na kushiriki katika masuala mazima ya maendeleo,”
alisema.
King
Nahh aliongeza kwamba, hisia za watu wengi hivi sasa zimelemaa kutokana
na kuishia kulaumu matatizo na vikwazo bila kutafuta suluhu ya
matatizo yao.
“Kila
mtu analaumu. Wa kwanza atalaumu, wa pili, wa tatu, wa nne, wa tano
mpaka wa sita. Wote wanaishia kulaumu jambo moja. Wengine wanaamini kuwa
hawezi kitu. Ila ukweli ni kwamba pale unapokuwa huwezi kitu kuna kitu
unaweza kufanya. Jamii ibadilike. Iache kulaumu,”alisema mtoto huyo na
kushangaza watu waliokwenda kumlaki.
Mkurugenzi
wa taasisi ya Wisdom Partners, Cynthia Henjewelle, alisema kuwa dhamira
kubwa ya kumleta mtoto huyo nchini ni kusaidia kubadili hisia za jamii
hasa watoto ili waweze kujiona kuwa sehemu ya jamii.
“King
Nahh ni miongoni mwa watoto wanaosifika hivi sasa duniani kutokana na
kipawa alichonacho. Wazazi wawalete watoto kesho Urafiki, ili waweze
kubadilishana mawazo. Pia wazazi wanakaribishwa kumsikiliza mtoto huyu
kuanzia saa tano asubuhi,”alieleza Henjewele.
MTOTO MWENYE KIPAJI CHA AJABU KUTOKA MAREKANI ATUA NCHINI LEO, KUFANYA KONGAMANO LA WATOTO NA WAZAZI KESHO JIJINI DAR ES SALAAM
Reviewed by crispaseve
on
11:59
Rating:
Post a Comment