UNESCO KUENDELEA KUSAIDIANA NA TANZANIA KUINUA ELIMU
Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akielezea
mantiki ya warsha ya wadau wa elimu kuhusu viwango vya umahiri wa Tehama
kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu Tanzania iliyofanyika mjini Bagamoyo,
mkoa wa Pwani mwishoni mwa juma.
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limesema
litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba
taifa linakuwa na wananchi wenye uwezo mkubwa wa kuvumbua na kutumia
elimu.
Kauli
hiyo imetolewa na Ofisa wa Unesco nchini Al Amin Yusuph wakati
akizungumza na washiriki wa kongamano maalumu wa kupitia waraka wa
mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.
Kongamano
hilo ni moja ya mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wenye
lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi
na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.
Mradi
huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa
ya Tehama na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
Ingawa
kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vya Tabora
na Monduli vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu
ambavyo vitaingizwa.
Mratibu
wa Kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akifafanua jambo kwa
wadau wa kongamano la kupitia kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini lililofanyika mjini Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa juma.
UNESCO KUENDELEA KUSAIDIANA NA TANZANIA KUINUA ELIMU
Reviewed by crispaseve
on
05:27
Rating:
Post a Comment