NEWZ ALERT AGNESS MASOGANGE AFARIKI DUNIA JIONI YA LEO
Msanii
Video Queen Agness Gerald (Masogange) amefariki Dunia jioni ya leo
katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo jijini Dar Es Salaam baada ya
jana kuzidiwa na kukimbizwa hospitalini hapo.
Taarifa kutoka kwa vyanzo vya uhakika vimeeleza kuwa Agness alizidiwa jana mapema na kukimbizwa katika hospitali hiyo kwa matibabu ya haraka,lakini kwa bahati mbaya mapema leo jioni alifariki Dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo,ambapo mpaka sasa haijainishwa wazi Ugonjwa uliokuwa ukimsumbua.
Aidha
Michuzi Blog imeshuhudia Mwili wa Marehemu Agness Masogange ukiondolewa
kituo cha Afya cha Dkt Ngoma na kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya
Taifa Muhimbili jioni hii.
Tutazidi kuwaleta taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu,
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-Amen
NEWZ ALERT AGNESS MASOGANGE AFARIKI DUNIA JIONI YA LEO
Reviewed by crispaseve
on
11:46
Rating:
Post a Comment