VETA MOSHI WAJIVUNIA AJIRA ZA MOJA KWA MOJA WANAZOPATA WANAOSOMA KATIKA CHUONI HAPO
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii, MOSHI
CHUO
cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Moshi kimeaanzisha na kuendeleza
mafunzo ya kozi ya Uzalishaji mvuke yenye fursa kubwa katika soko pamoja
na kozi ya mitambo katika uchimbaji wa madini ambao umetoa ndani na nje
ya nchi.
Akizungumza
na waandishi habari waliotembelea katika Chuo cha VETA Moshi, Kaimu
Mkuu wa Chuo hicho, Douglas Mlulla amesema moja ya mafanikio yao ni
kwamba vijana wanaosoma hapo wana uhakika wa ajira za moja kwa moja
kutokana na ushirikiano na kampuni za uchimbaji madini.
Amesema
VETA Moshi ni chuo kina kozi ambazo zina wigo mkubwa wa ajira katika
uchimbaji wa madini, pamoja kozi uzalishaji mvuke ambapo sehehu ya
viwanda vya vinywaji ni lazima kuwepo kwa wataalam wa kozi hiyo.
Hata
hivyo amesema mwitikio wa vijana ni mdogo kutokana na kutofahamu umuhimu
wa ufundi stadi ambao ndio unaajiri watu kwa sehemu kubwa, hivyo
ameashauri vijana kuchangamkia fursa hata kama anashahada ni vema
akaongeza na mafunzo ya ufundi stadi.
Pia amesemakozi ya Uendeshaji wa mitambomikubwa imeonekana kuvutia vijana wengi wakiwemo wasichana.Mmoja
wanafunzi wa kozi hiyo, Happiness Steven amesema yeye anashahada ya
kwanza rasilimali watu na baada ya kuona changamoto ya ajira ameamua
kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi na kufanikiwa kupata kazi katika
kiwanda na kuwa afisa uajiri katika kiwanda hicho.
Amesema
kozi ya uchomeleaji na uchongaji wa vyuma alivutiwa na kuamua kujiunga
nayo licha ya mtazamo uliokuwepo kwa muda mrefu kuwa hiyo ni kozi kwa
ajili ya wanaume.Amesema
waliohitimu Shahada wajiongeze katika ufundi stadi na hatimaye
changamoto ya ajira watakuwa wameimaliza kwani hakuna kazi isipokuwa ni
watu kuchagua kazi za kufanya kwa taaluma waliozonazo.
Kwa upande wa Mratibu
wa Mradi wa IMTT Chuo hicho,Theresia Mosha amesema ushirikiano kati yao
na kampuni za uchimbaji madini umetoa fursa vijana wengi waliopita
katika mradi huo pamoja na waliosomea kozi ya uzalishaji mvuke kupata
ajira.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Moshi , Douglas Mlulla akizungumza na waandishi habari walipotembelea chuo hicho kuhusiana na fursa ambazo zinapatikana katika chuo.
.Afisa Rasilimali Watu wa Kiwanda cha Press , Forge & Metal Works (PFM2000) na Munufaika mafunzo ya ufundi Stadi VETA Moshi, Happiness Steven akizungumza wa kuhusiana na vijana kuchangamkia kozi ya ufundi stadi licha ya kuwa na shahada walizozipata.
Munufaika mafunzo ya ufundi Stadi VETA Moshi Happiness Steven akionesha umahiri alioupata katika mafunzo ya ufundi Stadi katika chuo cha VETA Moshi.
Mwanafunzi wa kozi ya Mitambo Mikubwa,Happiness Rwechungura akioneha jinsi wanavypata mafunzo ufundi stadi katika chuo cha VETA Moshi.
Mkufunzi wa Kozi ya Mtambo wa kuzalishaji Mvuke , Mosana Marcus akionesha jinsi mtambo unavyoweza kuzalisha mvuke
VETA MOSHI WAJIVUNIA AJIRA ZA MOJA KWA MOJA WANAZOPATA WANAOSOMA KATIKA CHUONI HAPO
Reviewed by crispaseve
on
11:40
Rating:
Post a Comment