RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WAGENI MBALIMBALI IKULU AKIWEMO RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU BENJAMIN MKAPA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Ndg. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Mei, 2018
amekutana na kufanya mazungumzo na Wenyekiti watatu wa Jumuiya
za CCM, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Wenyeviti hao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Ndg. Edmund
Mndolwa, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg.
Gaudentia Kabaka na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)
Ndg. Kheri James.
Baada ya mazungumzo hayo viongozi hao wamesema wamekutana na
Ndg. Magufuli na kumueleza kuhusu maendeleo ya Jumuiya zao na kumpa
salamu kutoka kwa Rais wa Afrika Kusini Ndg. Cyril Ramaphosa na Rais wa
Zimbabwe Ndg. Emmerson Mnangagwa pamoja na viongozi wa vyama
tawala vya ANC cha Afrika Kusini na ZANU-PF cha Zimbabwe ambavyo ni
vyama rafiki vya CCM.
“Tumekuja kumueleza ziara yetu ilikuwaje lakini zaidi ya hapo sisi
kama wenyeviti wake wa Jumuiya tumekuja kuzungumza nae ili
tuweze kuendesha jumuiya zetu kwa ufanisi mzuri zaidi” amesema
Ndg. Mndolwa.
“Tumekuja na salamu kutoka kwa Marais wa Afrika Kusini na Zimbabwe,
wanasema wanatuheshimu sana na wanatutegemea sana, pia wametaka
urafiki wa vyama vyetu uendelee” amesema Ndg. Kabaka.
“Tumefikisha salamu za vijana wa CCM kwa vijana wa vyama rafiki
vya ANC na ZANU-PF na kimsingi vijana wa ANC na ZANU-PF wanatambua
mchango mkubwa wa CCM katika kufikisha mataifa yao kwenye mafanikio
makubwa ya uhuru na maendeleo waliyonayo leo” amesema Ndg. Kheri James.
Katika hatua nyingine Ndg. Magufuli amekutana na kufanya
mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu na Mwenyekiti Mstaafu
wa CCM Ndg. Benjamin William Mkapa na Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Bara) Ndg. Philip Mangula, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
25 Mei, 2018
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika mazungumzo na Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa
(kushoto) pamoja na Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara
Philip Mangula Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akijadiliana jambo na Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa
(kulia) pamoja na Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara
Phillip Mangula (kushoto) mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar
es Salaam.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wazazi (CCM) Dkt. Edmund Mndolwa, Mwenyekiti wa Umoja wa
Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka pamoja na Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James mara baada ya kumaliza
mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Dkt. Edmund Mndolwa, Mwenyekiti wa
Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka pamoja na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James mara baada
ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James mara baada ya kumaliza mazungumzo
yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa
Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wazazi (CCM) Dkt. Edmund Mndolwa mara baada ya kuwasili Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James Ikulu jijini
Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WAGENI MBALIMBALI IKULU AKIWEMO RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU BENJAMIN MKAPA
Reviewed by crispaseve
on
11:39
Rating:
Post a Comment