TCRA WATOA LESENI KWA WATOA HUDUMA ZA HABARI MTANDAONI
*Mkurugenzi TCRA asema 45 ndio wamekidhi vigezo kati ya waombaji 262
*Asema mchakato bado unaendelea, atoa sababu kuweke gharama za usajili
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.
MAMLAKA
ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania(TCRA)imesema leo ni siku muhimu
katika tasnia ya habari na utangazaji kutokana na kushuhudiwa wadau wa
habari wakiwa wamekamilisha hatua za usajili ili watambulike na kutumia
fursa hiyo ya utoaji na upashaji habari kupitia mtandao wa intanenti.
Kutokana
na kukamilisha mchakato huo TCRA imetoa leseni kwa watoa huduma wa
maudhui kwa njia ya mtandao wa intanenti 45 kati ya watoa huduma 262
walioomba na wengine kushindwa kutimiza vigezo vilivyowekwa.
Miongoni mwa waliopewa leseni baada ya kukamilisha taratibu hizo ni pamoja na Michuzi Media Group(MMG) inayoendesha Michuzi Blog na Michuzi TV.
Miongoni mwa waliopewa leseni baada ya kukamilisha taratibu hizo ni pamoja na Michuzi Media Group(MMG) inayoendesha Michuzi Blog na Michuzi TV.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi
James Kilaba wakati akikabidhi cheti cha usajili kwa wamiliki 45 wa
Blogs, Redio na televisheni za mtandaoni na kusema kuwa zipo faida
nyingi za habari na utangazaji kwa njia ya mtandao ambazo zinafahamika
kwa wengi.
"Kama
tunavyofahamu kwa miongo mingi sasa sekta ya habari na utangazaji
imekuwa ikipata habari kwa njia ya redio na televisheni kupitia majukwaa
mbalimbali kama mitambo iliyojengwa ardhini,Satellite na Cable.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba
akizungumza wakati wa utoaji wa leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa
njia ya mtandao , iliyofanyika leo katika ukumbu wa TCRA jijini Dar es
Salaam.
Katibu
wa Tanzania Bloggers Network (TBN) Krants Mwantepele akizungumza
kuhusiana na mwitikio ulionyeshwa kwa wamiliki kujisajili TCRA
iliyofanyika , jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Mhandisi
James Kilaba akikabidhi leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya
mtandao kwa Mmoja wa Wakurugenzi wa Michuzi Media Group (MMG), Ainde
Ndanshau katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba
akikabidhi leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa
Mkurugenzi wa Blogu ya Wananchi , William Malecela ‘LE MUTUZ ‘ Vkatika
hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Mhandisi
James Kilaba akikabidhi leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya
mtandao kwa Mwakilishi wa Mtandao wa Bongo 5, Yassin Ng’itu katika
hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba
akikabidhi leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa
Mmiliki wa Habari Mseto , Francis Dande katika hafla iliyofanyika katika
ukumbi wa TCRA , jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Mhandisi
James Kilaba akikabidhi leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya
mtandao kwa Mmiliki wa Radio Seven ya Mtandaoni, Atu Mandoza katika
hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es Salaam.
TCRA WATOA LESENI KWA WATOA HUDUMA ZA HABARI MTANDAONI
Reviewed by crispaseve
on
11:33
Rating:
Post a Comment