Header AD

Majeshi yajaribu kupindua Guinea-Bissau

Wanajeshi wamechukua udhibiti wa mji mkuu wa Guinea-Bissau katika kile kinachoonekana kuwa jaribia la mapinduzi.
Wanajeshi wa Guinea Bissau katika jaribio la mapinduzi
Mfulilizo wa sauti ya risasi ilisikika katika mji wa Bissau na pia katika makao ya Waziri Mkuu anayeondoka Bwana Carlos Gomes Junior.
Wanajeshi pia walichukuwa udhibiti wa Radio ya kitaifa na makao makuu ya chama tawala.
Katika awamu ya kwanza ya uchaguzi wa urais Bwana Gomes aliibuka mshindi japo hakufikisha idadi iliyohitajika.
Lakini kufukia sasa hatma ya Bwana Gomes haijulikani.
Na pia rais wa muda Bwana Raimundo Pereira hajulikani aliko.
Muungano wa mataifa ya mangaribi mwa Afrika ECOWAS imeshutumu kitendo hicho cha wanajeshi na kukitaja kama jaribia la mapinduzi.
Kufikia Ijumaa mkaazi mmoja aliambia BBC kuwa Televisheni na Radio ya kitaifa zilikuwa hazipeperushi matangazo.
Hata hivyo imeripotiwa kuwa hali imeanza kuwa shwari huku watu wakijitokeza kuendelea na shughuli zao.
Reviewed by crispaseve on 08:04 Rating: 5

No comments

Post AD