Header AD

RAIA WAWILI WA BURUNDI WAKAMATWA NA SILA KIGOMA

KAIMU KAMANDA KIHENYA KIHENYA AKIWAONESHA WAANDISHI WA HABARI SIRAHA MBILI ZA KIVITA AINA YA SMG ZILIYO KAMATWA
 
Na Pardon Mbwate na Felister Elias wa Jeshi la Polisi -Kigoma
 
Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma linawashikilia watu wanne wakiwemo wawili raia wa nchi jirani ya Burundi kwa tuhuma za kupatikana na silaha mbili za kijeshi aina ya SMG na risasi mbili.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP Kihenya wa Kihenya, amewataja Raia hao wa Burundi waliokamatwa kuwa ni Ndolimana Alfred Ndoli(29), mkaazi wa Lutana Kiharu na Bosco  Yohana Gabriel(35), mkaazi wa Kibimba Giharu ambao walikamatwa katika kijiji cha Nguruka silaha moja wakiwa na SMG moja yenye namba 56–2500509
 
Kamanda Kihenya amewataja Watanzania waliokamatwa sambamba na Warundi hao kuwa ni Matata Chubwa  Ntasamba(36), mkaazi wa kijiji cha Kitanga Wilaya ya Kasulu na Ndegeya Medard(28), mkazi wa kijiji cha Kitanga wilaya ya Kasuliu mkoani Kigoma walikamatwa katika Kitongoji cha Lugongoni tarafa ya Nguruka wakiwa na magazini mbili za SMG na moja kati ya hizo ikiwa na risasi mbili. 
 
Amesema kuwa silaha iyoyo na risasi ilipatikana katika kandokando ya mto Ruguzye uliopo katika pori la kijiji cha mabama wilayani Kinondo baada ya kutelekezwa na majambazi wasiojulikana kufuatia msako mkali unaoendelea mkoani humo wa kutafuta silaha na majambazi wa kutumia silaha.
 
Katika tukio lingine Kamanda Kihenye amesema mkazi mmoja wa Kitongoji cha Mrusi  mjini Kasulu, Elizabeth  Kanyungu(46), alikutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani ndani ya nyumba yake.
Reviewed by crispaseve on 08:03 Rating: 5

No comments

Post AD