GEEZ MABOVU ALAZWA BAADA YA KUUGUA GHAFLA MUDA MCHACHE KABLA YA KUFANYA SHOW MKOANI IRINGA.
Geez Mabovu.
Msanii wa Muziki wa Hip Hop Nchini, Geez Mabovu hali yake imeripotiwa kuwa sio nzuri baada ya kuugua ghafla wakati alipokuwa akisubiria kupanda jukwaani kufanya show, katika show hiyo Geez alikuwa na wasanii wenzake Songa na Jan B.
Kupitia mtandao wa Facebook, Rapa kutoka Tamaduni Muziki Songa aliweza kuwataarifu mashabiki na wapenzi wa burudani kuhusian na kile kilichotokea na hiki ndicho alichoandika.
“ASANTENI SANA IRINGA,SIKUTEGEMEA MNAPENDA HIP HOP KIASI KILE…MLITISHA SANA. ILA KUNA HABARI MBAYA NDUGU YETU GEEZ MABOVU HALI YAKE SIO NZURI AMELAZWA,NAOMBA TUMUOMBEE ARUDI KATIKA HALI YAKE YA KAWAIDA. ASANTENI”
GEEZ MABOVU ALAZWA BAADA YA KUUGUA GHAFLA MUDA MCHACHE KABLA YA KUFANYA SHOW MKOANI IRINGA.
Reviewed by crispaseve
on
21:09
Rating:

Post a Comment