Madonna na Brahim Zaibat
Mwanamuziki nguli wa miondoko ya Pop Duniani kutoka Marekani aliyepata kung’aa katika medani ya muziki wa kimataifa kwenye miaka ya 80 mwishoni mwa miaka ya 90, Madonna Louise Ciccone(55) a.k.a Lady Madonna hatimaye ametangaza rasmi kuvunja mahusiano ya kimapenzi na aliyekuwa serengeti boi wake Brahim Zaibat(25) ambaye ni densa katika uhusiano yaliyodumu ndani ya miaka tatu licha ya kwamba mwanamuziki huyo kukataa kuelezea sababu zilizochangia kuvunjika kwa penzi lao hilo
Kumbukumbu zinasema kwamba uhusiano kati ya wawili hao ulianza kugundulika rasmi mwaka 2010 baada ya wawili hao kuanza kuonekana katika hafla na matamasha mbalimbali wakiwa pamoja kama vile pea za viatu na mapema mwaka huu mitandao mbalimbali inayoandika habari za mastaa ilimnukuu Lady Madonna akisema kwamba uhusiano wake na serengeti boi wake kwani ni kama jinsi yalivyo mahusiano ya watu wengine licha ya kuwepo kwa tofauti kubwa ya umri na umaarufu mkubwa alionao.
Post a Comment