Papa Francis.
Papa mkuu wa kanisa katoliki Duniani, Jorge Mario Bergoglio(77) maarufu kwa jina la Papa Francis ametajwa katika jarida maarufu la Time kama Person of the year kwa mwaka wa 2013, hii itakuwa ni mara ya tatu kwa papa wa kanisa hilo katoliki kupewa heshima hii kubwa, ikumbukwe kwamba papa Francis alichaguliwa na jarida maarufu Duniani la Time mnamo mwezi wa tatu mwaka huu katika kipindi ambacho viongozi kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakipimwa ni kwa kiasi gani wanaweza wakakabilliana na changamoto zinazotokea katika jamii bila kutumia nguvu ya aina yoyote na kufanya jamii iweze kumkubali na kuwa na ushawishi mkubwa, hiyo ndio sababu hasa ya msingi iliyofanya Papa Francis aweza kutajwa kama Man Of The Year 2013.
Post a Comment