Watu 9 Wamefariki Dunia Papohapo na 30 Kujeruhiwa Katika Ajali Mkoani Lindi
BASI Likiwa limeanguka na maiti bado zilikuwa hazijatolewa chini

Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga akisimamia zoezi la kuinua basi hilo kwa ajili ya utoaji wa Maiti 9 za ajali hiyo.

Baadhi ya abiria ambao walikuwemo katika basi hilo wakiwa wametoka bila kujeruhiwa
----
Na Abdulaziz Video, Lindi
Watu 9 wakiwemo watoto 2 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 30
kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria la Alhamdulilah linalofanya
safari zake kutoka jijini Dar kwenda mkoani Mtwara kupinduka katika
kijiji cha Mambulu Manispaa ya Lindi.
Ajali hiyo iliyotokea mchana jana baada ya basi hilo kupishana na lori
na kupoteza mwelekeo na kupinduka hali ilichangiwa na mvua iliyokuwa
ikiendelea kunyesha.Hadi ninatoka eneo la tukio marehemu hao hawakuweza kufahamika kwa
haraka kutokana na kukatika viungo na tayari majeruhi na maiti wote wamefikishwa hospitali.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi,George Mwakajinga ambae
alikuwepo katika eneo la ajali hiyo hakuweza kuongea lolote kutokana na kutingwa na harakati za kuokoa majeruhi wa Ajali hiyo
Watu 9 Wamefariki Dunia Papohapo na 30 Kujeruhiwa Katika Ajali Mkoani Lindi
Reviewed by crispaseve
on
04:29
Rating:

Post a Comment