Header AD

BIRDMAN AMZAWADIA JUSTIN BIEBER BUGATTI.

Birdman na Justin Bieber
Birdman na Justin Bieber
Muanzilishi na mmiliki wa studio ya Cash Money, mjasiriamali na rapa Brayan Williams(45) ‘BirdMan’ amemzawadia mwanamuziki wa R&B, Justin Bieber gari ya kifahari aina ya ‘Bugatti Veyron’  yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 2 alilokuwa akitumia hapo awali.
“Uncle Stunna luv. My first Bugatti ♛ #generosity,” aliandika Justin Bieber kwenye ukurasa wake wa Instagram sambamba na kuweka picha ya mkoko huo wa bei chafu.
Katika picha ni gari aina ya Bugatti aliloposti Justin Bieber Instagram
Katika picha ni gari aina ya Bugatti aliloposti Justin Bieber Instagram baada ya kupewa kama zawadi na Birdman.
 Kwa wale wafuatiliaji ni kwamba,  gari alilopewa Justin Bieber ndio alilolitumia BirdMan  kwenye video  ya wimbo wake wa ‘Fire Flame’  iliyotoka  mwaka 2010. unaweza ukautazama mkoko huo wa bei mbaya hapo chini.
BIRDMAN AMZAWADIA JUSTIN BIEBER BUGATTI. BIRDMAN AMZAWADIA JUSTIN BIEBER BUGATTI. Reviewed by crispaseve on 02:08 Rating: 5

No comments

Post AD