GUINEA YATINGA ROBO FAINALI KWA BAHATI, MALI YAFUNGASHA VIRAGO
Timu
ya Guinea iliyotoka sare juzi kwa kufungana bao moja kwa moja na timu
ya Mali kwenye michuano ya soka ya kombe la AFCON, imetinga robo fainali
ya michuano hiyo baada ya kushinda kwa njia ya bahati nasibu
iliyofanywa na shirkisho la soka barani Afrika CUF.
Bahati nasibu hiyo imeamua nafasi ya
pili katika kudni D, baada ya nchi zote mbili kumaliza kwa pointi sawa
katika michezo mitatu waliyocheza, huku ivory Coast ikimaliza kileleni
mwa kundi hilo.
Guinea inatarajia kushuka dimbani
Februari mosi mwaka huu kumenyana na timu ya Taifa ya Ghana katikamchezo
wa robo fainali mjini Malebo nchini humo.
GUINEA YATINGA ROBO FAINALI KWA BAHATI, MALI YAFUNGASHA VIRAGO
Reviewed by crispaseve
on
02:14
Rating:
Post a Comment