USIHOFU NDUGU JITETEE HIVI UWAPO MAHAKAMANI
IMEANDALIWA NA MAWAKILI WETU
( 1 ) Kama unahojiwa na Wakili mahakamani usijibu bila kutafakari alichokuuliza.
( 2 ) Wakili asikuogopeshe kwa ukali anapokuuliza kwani
ukali hulenga kuleta paniki na kukusahaulisha ulichopanga kusema.
( 3 ) Usilazimishe kujibu kitu ambacho hukijui ni bora
kusema sijui kuliko kulazimisha kujibu.
( 4 ) Penda sana
kujiamini kwakuwa kujiamini hupunguza
uwezo wa Yule anayekuuliza, hata
awe Jaji/Hakimu.
( 5 ) Jitahidi kupata ushauri wa wanaojua sheria
kwa kila hatua unayopiga katika kesi.
( 6 )Kama we
ni shahidi hakikisha unajadiliana vya kutosha
na Yule unayemtolea ushahidi kabla
hamjaingia mahakamani.
( 7 )Usipaniki
kiasi cha kutoa neno lolote la kashfa ,kejeli,
au tusi mahakamani unaweza kuongeza kosa
la kuidharau mahakama.
( 8 )Katika
kesi ya jinai usikubali kosa haraka kabla hujajua kitaalam kosa hilo linaundwa na nini(vipengele vya kosa).
( 9 )Kama hukuelewa vizuri kosa ulilosomewa ni bora kukaa kimya, kwakuwa ukikaa kimya unaandikiwa umekataa kosa.
( 10 )Kanuni
ya sheria ni kuwa, Ni kazi ya aliyekushitaki kuthibitisha kwa ushahidi kuwa
umetenda kosa na si kazi yako
kuthibitisha kuwa haujatenda kosa.
( 11 )Katika
kesi ya jinai msikilize kwa makini anayekushitaki na hakikisha unapata lolote lenye kutia shaka katika maelezo yake
na iambie mahakama shaka hilo hii ni kwasababu
huwezi kuwa na hatia kama kuna shaka katika maelezo.
(12)Kama
ulitenda kosa katika harakati za kujitetea usidhuriwe iambie mahakama kuwa
ulitenda kosa ukijilinda(self defence) inaruhusiwa, hata kama uliua waweza kuachiwa.
( 13 )Kama
ndugu yako hana akili tinmamu na ametenda kosa iambie mahakama.Hii ni kwasababu
kutokuwa na utimamu wa akili ni kinga
inabidi aachiwe lakini hatarudi nyumbani atapelekwa vituo vya wasio na akili.
( 14 )Inakubalika
na ukaachiwa huru ukisema kuwa ulilazimishwa kutenda kosa kama
kweli ulilazimishwa.
( 15 ) )Inakubalika
na ukaachiwa huru kusema kuwa sikuwa eneo la tukio wakati
likitokea kama kweli haukuwapo.
( 16 )Kama
kosa ni kupita taa nyekundu ikiwaka barabarani,swali lako kwa shahidi traffic lilenge kumbana kama sehemu aliyokuwa amesimama
alikuwa na uwezo wa kuangalia vizuri na kutambua rangi za taa. Mfn. jua kali linawaka yeye ameuonaje
mwanga wa taa kutoka mbali.
( 17 )Ukipewa nafasi ya kumhoji shahidi muhoji
maswali mafupi. Mfn. ulikaa upande wa pili barabara, si ndio, jua kali lilikuwa
linawaka , si ndio, ulifanya kazi ya kuangalia magari mengine pia si ndio, na
mbele kulikuwa na miti si ndio, sasa kama hali ilikuwa hivyo uliwezaje kuona
taa nyekundu ikiwaka wakati nakatiza.
18 )Ukipewa
nafasi ya kumhoji shahidi wako uliyemleta katu usimuulize swali ambalo mlikuwa
hamjalijadili na hivyo hujui atatoa jibu gani.
( 19 ) Kama
wanaokushtaki wanashahidi na unamjua kuwa kuna kipindi aliwahi kuchangnyikiwa au
kufanya tukio lolote la uhalifu kabla,
ni nafasi nzuri kuhoji uwezo na uadilifu wake mpaka aaminike kwa anayoyatolea ushahidi leo.
.........ITAENDELEA
USIHOFU NDUGU JITETEE HIVI UWAPO MAHAKAMANI
Reviewed by crispaseve
on
23:27
Rating:
Post a Comment