Waziri Fenella Mukangara kufunga Mashindano ya Proin Women Taifa Cup Kesho
Hatimaye
kesho fainali ya Proin Women Taifa Cup itafanyika katika uwanja wa Azam
Complex Chamanzi kwa kuzikutanisha timu za Pwani na Temeke huku Mshindi
wa Kwanza katika Michuano hiyo ataondoka na Kitita cha Shilingi za
Kitanzania Milioni 3 huku mshindi wa Pili akiondoka na Milioni 1 na
Mshindi wa Tatu akiondoka na Kitita cha Milioni 1.
Mashindano
ya Women Taifa Cup ni mashindano ya kwanza kufanyika Nchini Tanzania
huku yakiwa yamedhaminiwa na Kampuni ya Proin Promotions na Azam.
Katika fainali hiyo mashabiki wataingia Bure huku mechi hiyo ikirushwa live na Azam TV.
Mgeni
rasmi katika Fainali hiyo ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mh
Dkt Fenella Mukangara ambae atafunga mashindano hayo katika dimba la
Azam Complex ambapo mechi hiyo ya fainali itaanza kutimua vumbi saa
10:15 Jioni huku Jonesia Rukyaa refarii mwenye beji ya fifa ndiye
atakepuliza kipenga akisaidiwa na Hellen Mduma, Agness Alphonce na
Mwanahamisi Matiku huku kamisaa wa fainali hiyo anatarajiwa kuwa Ingridy
Kimaro.
Katika Mechi ya Kumtafuta mshindi wa tatu timu ya Ilala itamenyana na Kigoma ambapo mchezo huo utaanza saa 8 Mchana.
Waziri Fenella Mukangara kufunga Mashindano ya Proin Women Taifa Cup Kesho
Reviewed by crispaseve
on
00:32
Rating:
Post a Comment