MISS EAST AFRICA 2012- UGANDA
PRESS RELEASE
MISS EAST AFRICA 2012
Washiriki watakaoziwakilisha Nchi zao katika fainali mashindano ya Miss East Africa 2012 wanaendelea kutangazwa katika mchujo ulioendeshwa na kampuni ya East Africa gazelle ya Nchino humo.
Mrembo aliyetangazwa mwishoni mwa wiki ni Miss Ayisha Nagudi (23) kutoka Nchini Uganda atakayeiwakilisha Nchi hiyo katika fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012.
Miss Ayisha Nagudi ana urefu wa 1.82m ni mwanafunzi wa mwaka pili katika chuo kikuu cha Makelele jijini Kampala, ambapo anasomea degree ya Education
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 ambazo huandaliwa na kumilikiwa na Kampuni ya Rena Events Ltd, zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.
Reviewed by crispaseve
on
08:22
Rating:
Post a Comment