Wadau kibao wajitokeza Kuona Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ulioonyeshwa na DStv kwenye Kiota cha Samaki Samaki Mlimani city jijini Dar
Meneja Mauzo wa Kampuni
ya Multichoice Tanzania ambao ni wasambazaji wakuu wa Ving'amuzi vya
DStv,Salum Salum (kulia) akizungumza na Wapenzi wa soka walikuwa
wamefurika kwa wingi kwenye kiota cha Samaki Samaki,Mlimani City jijini
Dar es Salaam jioni ya leo kwa kushuhudia Ufunguzi wa Mashindano ya
Kombe la Mataifa ya Afrika (yanayofanyika huko nchini Afrika ya
Kusini),ambapo DStv waliendesha zoezi hilo na pia kuchezesha bahati
nasibu kwa wapenzi hao wa Soka walikuwepo hapo.Kushoto ni Meneja
Mahusiano wa Multichoice Tanzania,Barbara Kambogi
Meneja Mauzo wa Kampuni
ya Multichoice Tanzania,Salum Salum na Meneja Mahusiano wa kampuni
hiyo,Barbara Kambogi wakichezesha droo ya bahati nasibu ya Shinda
King'amuzi cha DStv katika kipindi hiki cha Mashindano ya Kombe la
Afrika.
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya
Multichoice Tanzania,Barbara Kambogi (kushoto) akikabidhi King'amuzi
hicho kwa Mshindi wa bahati nasibu hiyo,ambaye ni Mwanalibeneke wa
Libeneke la Mtaa kwa Mtaa Blog,Othman Michuzi (pili kulia) mara baada ya kuibuka kidedea.(Duuhh.....!! jamaa anazali huyu!).
Baadhi ya Wadau wa DStv
wakifuatilia Mtanange wa Ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika,kati ya
timu ya Cape Verde na Afrika ya Kusini ambao ulimalizika kwa kutoka
suluhu ya bila kufungana.
Wadau kibao toka maeneo mbali
mbali ya jiji la Dar wakiwa kwenye Kiota cha Samaki Samaki jijini Dar
kufuatilia Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika uliokuwa
ukirushwa moja kwa moja kupitia DStv kutokea nchini Afrika ya Kusini
yanakofanyika Mashindano hayo.
Reviewed by crispaseve
on
08:59
Rating:
Post a Comment