MABONDIA WA TANZANIA WAFUNGWA MIAKA 15 NCHINI MAURITIUS.
Pichani ni mabondia wa Tanzania ambao wamefungwa kifungo cha miaka 15.
Mabondia hao ni Case Ramadhani Fills, Nathanael Elia Charles, Ally Rajabu Msengwa na Petro Charles Mtagwa.
Wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa, wote walikiri makosa ya
kuingiza mihadarati hiyo nchini Mauritius wakati walipokwenda kushiriki
mashindano ya ndondi barani Afrika mwaka 2008.
Wakiwa mbele ya Jaji, waliiambia mahakama kuwa walilazimika
kuingia katika biashara hiyo haramu kutokana na hali zao za maisha kuwa
maskini.
“Tunaomba radhi kwa taifa la Mauritius”, waliiambia mahakama.
“Tu watu maskini na tunategemewa na familia, watoto na wazee wetu wanaotugemea.”
“Kwa dawa hizi tungepata kiasi cha Pauni £4,000″. walisema
Jaji Benjamin Marie Joseph alisema katika kutoa adhabu hiyo yote
hayo ameyafikiria, kwani walitoa ushirikiano mzuri wakati wote wa
uchunguzi wa kesi hiyo, kulikowezesha hata wafanyabiashara hiyo, raia wa
Mauritius kukamatwa.
Wamekuwa mahabusu kwa siku 1,722, sawa na miaka miatano, hivyo
watatumikia miaka kumi iliyobakia jela. Pia watatakiwa kulipa faini ya
pauni £1,600 na gharama nyingine za uendeshaji wa kesi hiyo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa BBC nchini Mauritius Yasine
Mohabuth in Mauritius, Jaji aliwashutumu kwa kuukosea umma wa Mauritius
kwa kuingiza dawa hizo za kulevya aina ya heroin.
Mabondia hao waliwasili Mauritius tarehe 10 Juni 2008 na kuweza
kupita uwanja wa ndege bila kunaswa hadi walipokamatwa katika hoteli
waliyofikia ya Quatre Bornes.
Kwa pamoja walimeza gram 4639.04 za heroin zikiwa katika vifuko 358 vijulikavyo kama pipi.
Picha na habari : bbc swahili
Reviewed by crispaseve
on
13:16
Rating:
Post a Comment