BONDIA FRANCIS ”SMG” CHEKA AMCHAPA MMAREKANI PHIL WILLIAMS KWA POINT.
Bondia Francis Cheka wa Tanzania
(kulia) akimuadhibu mpinzani wake Mmarekani, Phill Williams, wakaati wa
pambano lao la raundi 12 la kuwania Ubingwa wa Dunia uzito wa Super
Middle (WBF) lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku
huu. Katika pambano hilo Bondi Mtanzania Francis Cheka ameweza
kumgalagaza kwa Pointi mpinzani wake na kutwaa ubingwa huo.
*******************
Na Mwandishi Wetu
HATA hivyo pambano hilo pamoja
na yale ya utangulizi yaliingia dosari baada ya wachezaji kama Alfonce
Mchumiatumbo, aliyekuwa akizichapa na Chupac Chipindi katika pambano lao
la utangulizi la raundi sita, kugoma kupanda ulingoni kwa kile
walichokuwa wakieleza mabondia hao kuwa wanahitaji kumaliziwa pesa zao
za mkataba wa kucheza mechi hizo kabla ya kupanda ulingoni.
Nao mabondia Mada Maugo na
Thomas Mashali, pia waligoma kupanda ulingoni wakishinikiza kumaliziwa
pesa zao kwanza jambo ambalo lilifanya kuzua taflani ukumbini hapoa huku
mapambano yakichelewa kuanza.
Ilipofika muda wa Cheka kupanda
ulingoni pia alisikika mtangazaji akimuita muandaaji wa mapambano hayo
ili kufika chumba alichokuwa Bondia mtanzania, Francis Cheka ili
kumalizana naye mkwanja ili akubali kupanda ulingoni.
Alisikika Cheka akimuwakia
muandaaji huyo kuwa, ” Nini Mmarekani hata angekuwa Mchina, nimalizie
changu kwanza ili nipande ulingoni, ambalo pia lilichukua muda wa
majadiliano hadi kuingiliwa kati na wadhamini na wadau wa ngumi
waliotangaza kujikomiti kulipa pesa hizo wanazodai mabondia, ndipo
mabondia hapo wakapanda ulingoni.
Aidha katika pambano la raundi
10 la mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali la kuwania Ubingwa wa WBF wa
Afrika, Thomas Mashali ameweza kumshinda kwa pointi 2 tu mpinzani wake
Mada Maugo na kutwaa Mkanda huo wa ubingwa wa WBF wa Afrika.
Na katika pambano la Utito wa
Juu la utangulizi la Raundi sita kati ya Bondia Alfonce Mchumiatumbo na
Chupac Chipindi, Mchumiatumbo amemchapa kwa KO mpinzani wake katika
raundi ya tano, baada Chupac kunyoosha mikono juu kuashiria na wasaidizi
wake kutupa taulo ulingoni kuashiria kushindwa kumalizia mchezo huo.
Waziri wa Habari, Fenella
Mukangara (katikati) akipozi na mabondia Phill na Cheka, ikiwa ni ishara
ya ufunguzi wa pambano hilo la kimataifa.
Waziri wa Habari, Fenella
Mukangara (wa pili kushoto) akimvisha Mknda wa Ubingwa wa Dunia wa WBF
Bondia Francis Cheka baada ya kumchapa kwa Pointi mpinzani wake
Mmarekani, Phill Williams, katika pambano lao la raundi 12 lililofanyika
kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu.
Mashabiki wa Cheka wakifurahi na kumbeba baada ya kutangazwa mshindi.
Bondia Mmarekani Phill Williams
(kulia) akichapana na Francis Cheka wa Tanzania katika pambano lao
lililomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mabondia hao wakiliana Timing…….
Cheka (kulia) na Phill wakichapana……
Cheka (kulia) na Phill,wakiendelea kuchapana
We subiri inakuja hiyooooo
Sehemu ya mashabiki wa mchezo huo waliofurika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kumshuhudia Cheka akimchakza Mmarekani.
Sehemu ya mashabiki wa mchezo huo waliofurika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kumshuhudia Cheka akimchakza Mmarekani.
Baadhi ya wageni waalikwa walioshuhudia mchezo huo.
Bondia Mada Maugo (kulia) akimwadhibu mpinzani wake, Thomas
Mashari kwa konde zito wakati wa
pambano lao la raundi 10 la kuwania ubingwa wa Dunia wa WBF, ambapo
Mashali ameibuka mshindi kwa
Pointi dhidi ya Maugo.
Picha kwa hisani ya Sufiani Mafoto Blog, Respect.
Reviewed by crispaseve
on
02:07
Rating:
Post a Comment