LADY JAYDEE AWATAJA WAIMBAJI WAPYA WA MACHOZI BAND.

Baada ya misukosuko ya hapa na pale kuikumba band ya Machozi
ambayo inamilikiwa na mwanadada Lady Jay Dee, hatimaye wamepatikana
waimbaji watatu waliopatika katika zoezi la kutafuta vipaji vya kike na
kwa taarifa ni kwamba tayari wameshajiunga na bendi hiyo inayofanya
vizuri hapa nchini.
Akitoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa mashabiki katika mtandao wa Facebook, Jay Dee a.k.a Anaconda aliandika hivi. ”Katika
kutafuta vipaji vya kike, nilifanikiwa kupata wasichana watatu ERICA,
CATHERINE a.k.a Chikitita na ANNA na tayari wamekwisha jiunga na Machozi
Band na wako vizuri sana… Picha na maelezo vitafuata kabla ya ufunguzi
wa Nyumbani Lounge Wanawake wakiwezeshwa wanaweza”. Hivyo kwa wale wapenzi wa burudani na TeamAnaconda wakae mkao wa kula na kuweza kupata ladha mpya kutoka kwa waimbaji hao wapya
LADY JAYDEE AWATAJA WAIMBAJI WAPYA WA MACHOZI BAND.
Reviewed by crispaseve
on
13:52
Rating:

Post a Comment