Mazoezi ya Miss Sinza kuanza Mei 5 kwenye ukumbi wa Meeda, Sinza
Prisca Clement katikati mara baada ya kushinda taji la vipaji katika mashindano ya Miss Tanzania 2013
MAZOEZI
ya warembo watakaowania taji la urembo la Sinza, Miss 2014
yataanza Mei 5 kwenye ukumbi wa Meeda uliopo Sinza Mori na Lufungila
jijini. Taji
la Miss Sinza linashikiliwa na Miss Tanzania, Prisca Clement alimaliza
katika hatua ya 10 bora katika mashindano ya mwaka jana ya Miss Tanzania
na pia alishinda taji la mrembo mwenye kipaji katika mashindano hayo.
Mratibu
wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa maandalizi ya mazoezi
hayo yamekamilika na yatasimiwa na kamati ya maandalizi huku ikitafuta
mwalimu kwa ajili ya kuwanoa.
Majuto
alisema kuwa warembo waliowahi kushiriki mashindano hayo wanaruhusiwa
kuja kutoa sapoti kwa warembo wapya na kamati yao itawapa nafasi ya
kuwafundisha warembo wapya ili kuwapa ‘mbinu’ mbali mbali za mashindano
hayo. Alisema
kuwa fomu za kuomba kushiriki katika mashindano hayo zinapatikana
kuanzia leo (Ijumaa) maduka ya Zizzou, Sinza Afrika Sana, Meeda, Ofisi
za Miss Tanzania na Ofisi za gazeti la Mwananchi (Tabata reline.
“
Lengo letu kubwa ni kurudisha hadhi ya Miss Sinza, Kinondoni katika
mashindano ya mwaka huu, tumejipanga kulinda heshima yetu na tunaamini
titafanikiwa kwa heshima ya wakazi wa Sinza, Kinondoni na Tanzania kwa
ujumla,” alisema Majuto.
Alisema
kuwa wanawakaribisha warembo wanaotaka ‘kupata taji’ kuchukua fomu zao
ambazo zinatolewa bure. Majuto pia aliwaomba wadhamini wanaotaka
kujitangaza kupitia mashindano yao wanaruhusiwa kuja kudhamini
mashindano hayo na milango ipo wazi.
Mazoezi ya Miss Sinza kuanza Mei 5 kwenye ukumbi wa Meeda, Sinza
Reviewed by crispaseve
on
16:06
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
16:06
Rating:


Post a Comment