Header AD

UTUMISHI YAIBUKA KINARA WA MPIRA WA PETE MASHINDANO YA MEI MOSI 2014

Fatuma Machenga (GS) mfungaji bora katika Mpira wa Pete wa mashindano ya Mei Mosi 2014 akiwa na kikombe baada ya kutangazwa rasmi katika hafla fupi iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuru mjini Morogoro.
Baadhi ya wachezaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (jezi za kijani) wakishangilia kwa kutawazwa mabingwa wapya wa Mpira wa Pete Mei Mosi 2014 kwa kuifunga timu ya Uchukuzi. Mashindano hayo yalimalizika jana jioni katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. 
Baadhi ya wachezaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi Umma, pamoja na mashabiki wao wakipongezana baada ya kuibuka mabingwa wapya wa Mpira wa Pete kwa kuifunga Uchukuzi katika mashindano ya Mei Mosi 2014 yaliyomalizika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mabingwa wapya wa Mei Mosi 2014, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika mazoezi mepesi kabla ya mchezo ambao waliifunga Uchukuzi na kunyaukua kombe la Mei Mosi 2014 iliyochezwa uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Sophia Komba akijiandaa kumdhibiti mchezaji wa Uchukuzi (C) (mwenye mpira) katika mechi ya fainali iliyochezwa katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Hekaheka ya kuwania mpira baina ya wachezaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (jezi za kijani) na Uchukuzi (jezi za bluu) katika mechi ya fainali ya Mei Mosi 2014 iliyochezwa jana uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Na. James Katubuka

Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma imetawazwa rasmi kuwa bingwa wa mpira wa Pete wa Mashindano ya Mei Mosi 2014.

Utumishi imefanikiwa kuwa bingwa baada ya kuisambaratisha timu ya Wizara ya Uchukuzi kwa ushindi wa magoli 33 dhidi ya 21. Mchezo huo wa fainali ulifanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Katika mchezo huo mchezaji Fatuma Machenga (GS) wa Ofisi ya Rais Utumishi ndiye aliyekua tishio kwa kuongoza wachezaji wa timu yake kufanikisha ushindi huo. 

Mchezaji Subira Jumanne (WA) wa Uchukuzi akizungumzia hali ya mchezo baada ya mpira kumalizika alisema kuwa mchezo ulikuwa mgumu na wapinzani wao walikua wamejiandaa vyema.
 “Naamini wakati wa mashindano mengine tutafanya vizuri kwa kujiandaa vyakutosha, asiyekubali kushindwa si mshindani” Subira alisema.

Wakati huohuo, Fatuma Machenga (GS) wa Utumishi ameibuka kuwa mfungaji bora wa mpira wa Pete katika mashindano ya Mei Mosi 2014 kwa kufunga jumla ya magoli 136.
 “Tutahakikisha kuwa mwakani tunapambana zaidi kwa kufanya mazoezi ya kutosha ili kutetea ubingwa wetu” Machenga alisema.

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imenyakua kombe hilo lililokuwa likishikiliwa na timu ya Wizara ya Ulinzi iliyokuwa bingwa katika mashindano yaliyopita Mwaka 2013. 
Mshindi wa Pili kwa mwaka 2014 ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mashindano hayo yalimalizika jana katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
UTUMISHI YAIBUKA KINARA WA MPIRA WA PETE MASHINDANO YA MEI MOSI 2014 UTUMISHI YAIBUKA KINARA WA MPIRA WA PETE MASHINDANO YA MEI MOSI 2014 Reviewed by crispaseve on 04:33 Rating: 5

No comments

Post AD