Rais Kikwete aongoza Harambee ujenzi wa Kanisa la KKKT Bumbuli
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wimbo wa wanabumbuli mara baada ya
kuwasili katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip kwa ajili ya harambee
ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Kilutheri la Bumbuli, Kushoto ni askofu
mkuu wa KKKT DKt.Gerhas Malasusa, Watatu Kulia ni Dkt.Steven Munga wa
Lushoto na kulia ni mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na teknolojia Mh.January Makamba Katika harambee
hiyo jZaidi ya Shilingi milioni mia tatu zilipatikana
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watu
walioshiriki katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la KKKT
Bumbuli jana iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip jijini
Dar es Salaam jana jioni.Walioketi mbele Wapili kushoto ni Mkuu wa
Kanisa la KKKT Tanzania Askofu Dkt. Gerhaz Malasusa,Askofu wa Lushoto
Steven Munga(Wanne kushoto) na Watano kushoto ni Mbunge wa Bumbuli
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Mh.January Makamba.Zaidi ya Shilingi milioni mia tatu zilikusanywa
katika harambee hiyo ikiwa ni ahadi,vifaa vya ujenzi na fedha taslimu .
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Naibu waziri Mawasiliano
Sayansi na Technolojia na mbunge wa Bumbuli January Makamba wakati wa
harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Bumbuli Shughuli hiyo
imefanyika katika Hotel ya Golden Tulip
.Picha na Freddy Maro
Rais Kikwete aongoza Harambee ujenzi wa Kanisa la KKKT Bumbuli
Reviewed by crispaseve
on
02:31
Rating:

Post a Comment