RAPA T.I ACHAPANA MAKONDE NA BONDIA FLOYD MAYWHEATHER, WIVU WATAJWA
Rapa maarufu anayetokea katika mji wa Atlanta, Georgia
‘Clifford Joseph Harris, Jr’ AKA T.I amejikuta akiingia kwenye ugomvi
na aliyekuwa rafiki yake bondia milionea ‘Floyd Money Maywheather Jr‘ asiye na rekodi ya kupigwa hata pambano moja Jumapili iliyopita jijini Las Vegas nchini Marekani wakati wa Memorial Day Weekend.
Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo kwenye mgahawa wa
FatBurger sehemu ulipotokea ugomvi, walidai kuwa chanzo ni mke wa T.I
anayeitwa Tiny kuonekana akiwa bege kwa bega na Maywheather kitendo
kilichoonekana kumkera T.I na kuamua kumfuata bondia huyo sehemu
aliyokuwa amekaa na kumuanzisha timbwili hali iliyopelekea mabaunsa
kuingilia kati na kufanikiwa kuwatenganisha mastaa hao na kila mmoja
kuchukua njia yake.
mke wa T.I mwanamama ‘Tiny’ akimsikiliza kwa makini bondia Floyd Maywheather muda mfupi kabla ya tukio la ugomvi kutokea.
Baadhi ya vyanzo vimedai kuwa T.I amekuwa akitilia shaka
ukaribu wa mkewe na Maywheather huku ikitajwa kuwa sio mara ya kwanza
kwa Rapa huyo kumlalamikia Maywheather kutembea na mama watoto wake
licha ya bondia huyo kukanusha mara zote na kudai kuwa amekuwa
akifahamiana na Tiny kwa kitambo kirefu.
”I’m not sleeping with that girl [Tiny] and I told that man
before. But if I was, talk to her about that, don’t talk to me about
that. But I’m not going to be disrespectful because I’m not going to
sleep with a married woman. Now if she was divorced”…alisema Maywheather
Pichani
ni Ujumbe na Picha aliopost mke wa T.I akifungukua kuwa yeye ni shabika
mkubwa wa Maywheather na timu yake ya The Money Team(TMT)
Hata Hivyo imefahamika kuwa Tiny alikwenda mjini Vegas
mwenyewe baada ya kupewa shavu la kusimamia mipango ya shereehe ya siku
ya kuzaliwa ya binti wa bondia huyo aliyepiga nae picha muda mfupi
kabla ya ugomvi na kisha kutupia kwenye ukurasa wake wa Instagram na
kuandika ”My New Boo” kitendo kilichozidi kumtia hasira mumewe.
Tazama Video hapo chini uone jinsi ugomvi ulivyokuwa
RAPA T.I ACHAPANA MAKONDE NA BONDIA FLOYD MAYWHEATHER, WIVU WATAJWA
Reviewed by crispaseve
on
12:53
Rating:
Post a Comment