Mwasisi wa Swahili Blues Leo Mkanyia Azidi Kutikisa Kimataifa

Siku
chache zilizopita, Leo alirekodi wimbo wake mpya uitwao 'Pamoja.'
Miongoni mwa yatakayoonekana katika video ya wimbo huo ni performance ya
kihistoria ya msanii huyo katika moja ya vyuo vikuu vikubwa hapa
Uingereza, Nottingham University, ambapo Leo alifanikiwa kuwaimbisha
Kiswahili baadhi ya wahadhiri na wanafunzi wa chuo hicho kikuu. Katika
shughuli hiyo, Leo aliimba na kwaya ya Nottingham Academy.
Kinachomfanya
Leo kuwa msanii wa kipekee kutoka Tanzania kuwa na fursa kubwa ya
kutawala anga za muziki kimataifa ni ukweli kwamba amefanikiwa kuanzisha
kitu kipya- muziki aina ya Swahili Blues- na ambao tayari umeanza
kukubalika kimataifa.
Pamoja
na kufanya vizuri kimataifa, Leo bado anathamini asili yake. Kama video
ya pili inavyoonyesha, Leo alifanya mahojiano na mtandao mkubwa na
maarufu wa burudani Tanzania na Afrika kwa ujumla wa Bongo5. Kadhalika, msanii huyo anapata sapoti kubwa kutoka kwa mmoja wa waasisi wa muziki wa Hip-Hop nchini Tanzania, lejendari @XamiaSiku4Saa4
wa kundi maarufu kabisa la Kwanza Unit. Ieleweke kwamba katika shughuli
za muziki, kupata 'endorsement' ya mkongwe wa muziki ni uthibitisho
kuwa msanii husika anafanya kazi nzuri mno.
Kama Watanzania, tuna wajibu na kila sababu ya kumuunga mkono Leo, kwani sio tu anaitangza Tanzania yetu bali pia anautambulisha utamaduni wetu-kwa maana ya lugha ya Kiswahili- kupitia muziki wake wa Swahili Blues.
Unaweza kufuatilia maendeleo yake ya kimuziki kwa akaunti zake mbalimbali za mitandao ya kijamii: Twitter na Facebook na katika tovuti yake sambamba na ukurasa wake wa YouTube
Kama Watanzania, tuna wajibu na kila sababu ya kumuunga mkono Leo, kwani sio tu anaitangza Tanzania yetu bali pia anautambulisha utamaduni wetu-kwa maana ya lugha ya Kiswahili- kupitia muziki wake wa Swahili Blues.
Unaweza kufuatilia maendeleo yake ya kimuziki kwa akaunti zake mbalimbali za mitandao ya kijamii: Twitter na Facebook na katika tovuti yake sambamba na ukurasa wake wa YouTube
Mwasisi wa Swahili Blues Leo Mkanyia Azidi Kutikisa Kimataifa
Reviewed by crispaseve
on
00:16
Rating:

Post a Comment