Coastal Union Kukipiga na AFC ya Arusha kusheherekea miaka hamsini na nne ya Uhuru wa Tanzania.
TIMU ya
soka Coastal Union ya Tanga inatarajia kusheherekea miaka hamsini na nne ya
Uhuru wa Tanzania kwa kucheza mechi ya kirafiki na timu ya AFC ya Arusha
itakayochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Desemba 9 mwaka huu.
Mechi hiyo
ni maandalizi kwa timu hiyo kujiandaa na mechi zake za Ligi kuu soka Tanzania
bara baada ya mapumziko ya siku kumi kutokana na Ligi kuu kusimama kwa muda
ambapo itaendelea Desemba 26 mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa
mechi hiyo itakuwa ni muhimu kwa timu hiyo kujitayarisha kwa ajili ya raundi
inayofuata kwenye michuano hiyo.
Amesema
kuwa baada ya kumalizika mechi hiyo wataangalia uwezekano wa kutafuta mechi
nyengine ya majaribio kabla ya kuanza ligi hiyo ambayo msimu huu imeonekana
kuwa na upinzani mkubwa
Aidha amesema
kuwa timu hiyo ya AFC yenye makazi yake Mkoani Arusha inatajiwa kuwasili mkoani
Tanga Desemba 8 mwaka huu kwa ajili ya mtanange huo lengo likuwa kuziandaa timu
zote mbili kwa mashindano yanayowakabili.
Amesema kuwa
mechi hiyo ina umuhimu kwa timu zote mbili sisi ni kujiandaa na Michuano ya
Ligi kuu Tanzania bara raundi inayofuata na wapinzania wetu wanajiandaa na Ligi daraja la kwanza hapa
nchini.
Hata hivyo
amesema kuwa mazoezi ya timu hiyo yameendelea kushika kasi kwenye viwanja vya
Mkwakwani mjini Tanga baada ya wachezaji wote waliokwenda mapumziko kurejea kwa
asilimia kubwa.
Coastal Union Kukipiga na AFC ya Arusha kusheherekea miaka hamsini na nne ya Uhuru wa Tanzania.
Reviewed by crispaseve
on
06:47
Rating:
Post a Comment