KAMATI YA MUDA YA BLOGGERS TANZANIA YAANZA KUPITIA RASIMU YA KATIBA
Mwenyekiti
wa Muda wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania
(Bloggers), Joachim Mushi (kulia), akizungumza wakati akifungua
majadiliano kwa wajumbe wa kamati ya muda ya Jumuiya ya wamiliki wa
mitandao ya jamii Tanzania ya kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar
es Salaam leo.
Majadiliano
hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa
hatua za usajili wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania
(Bloggers). Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo ya muda kutoka Zanzibar,
Othman Maulid "Mapara".
Katibu
Msaidizi wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim
Mwasha (kushoto),akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo wakati wa mapitio
ya rasimu hiyo. Kulia ni Mjumbe wa Kamati, Henry Mdimu.
Mwenyekiti
wa Muda wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania
(Bloggers), Joachim Mushi (wa pili kushoto), wakati akifungua
majadiliano kwa wajumbe wa kamati ya muda ya Jumuiya ya wamiliki wa
mitandao ya jamii Tanzania ya kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar
es Salaam leo. Majadiliano hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba
kabla ya kuipitisha kwa hatua za usajili wa Jumuiya ya Wamiliki wa
Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers). Kutoka kushoto ni Mjumbe, Othman
Maulid, Katibu Msaidizi wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania ,
Shamim Mwasha, Henry Mdimu (Mjumbe), Mariam Ndabaganga (Mjumbe) na
William Malecela (Mjumbe).
Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao uliofanyika katika Mgahawa wa MOG Lounge, jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
KAMATI YA MUDA YA BLOGGERS TANZANIA YAANZA KUPITIA RASIMU YA KATIBA
Reviewed by crispaseve
on
07:16
Rating:
Post a Comment