Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere arejea CCM.
Mbunge
wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Leticia
Nyerere akinyanyua mikono ikiwa ni sehemu ya ishara ya kuondoka katika
chama hicho na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati alipokutana na
waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo leo jijini
Dar es Salaam.
Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere akifafanua jambo kwa waandishi habari juu ya kuondoka katika chama hicho.
Waandishi
wa habari wakifuatilia kwa umakini maelezo ya Mbunge wa Viti Maalum
Chadema,Leticia Nyerere juu ya kuhama kwake katika chama hicho katika
ukumbi wa idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi
akiuliza swali kwa Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere ambaye
leo alikutana na waandishi habari juu kuhama chama hicho na kurejea CCM
katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo
jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii.
MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa
Mara ,Leticia Nyerere amengatuka rasmi leo katika chama hicho na kudai
kuwa anarudi nyumbani katika chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza
na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya habari maelezo
jijini Dar es Salaam,Leticia amesema kuwa katika suala la kuhamia
Chadema hakutafakari kwa kina labda angetafakari asingeweza kwenda huko.
Amesema mchango wake unatambulika sasa anaweza kutumikia CCM nje bila ya kuwa mbunge na kuweza kuleta maendeleo kutokana na uwezo wake katika masuala ya siasa.
“Moyo
wangu umekuwa ukisoneneka kutokana na kukaa Chadema na kuacha kukaa
katika chama kilichonilea na kunisomesha hadi nje ya nchi ,sasa nasema narudi nyumbani kutumikia”amesema Leticia.
Leticia
amesema kwenda Chadema alifanya ujinga bila kutafakari na hawezi
kulaumu dhamira yake mpya kurudi katika chama kilichompa makuzi yote na
atatumikia CCM kwa kasi mpya na kuleta maendeleo chanya kutokana na kile
ambacho amekuwa akitoa katika michango ya bunge.
Amesema wapinzani wote wa zamani walikuwa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM)hivyo katika maamuzi yake ya kwenda Chadema hayakuwa shahihi.
Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere arejea CCM.
Reviewed by crispaseve
on
05:39
Rating:
Post a Comment