MTANZANIA ASHINDA MEDALI MBILI ZA DHAHABU SWAZILAND.
Bingwa wa mita 1500,
Basil John kutoka Jeshi la Polisi Tanzania akimaliza mbio katika uwanja wa
Mavuso mjini Mbabane Swaziland ambapo alifanikiwa kuchukua nafasi ya katika michezo ya majeshi ya Polisi kwa nchi
za Kusini mwa Afrika(SARPCCO) inayoendelea nchini Swaziland.(Picha na Frank
Geofray wa Jeshi la Polisi-Swaziland)
Bingwa wa mita 1500,
Basil John kutoka Jeshi la Polisi Tanzania akipongezwa na Mkuu wa Jeshi la
Polisi la Swaziland baada ya kumvalisha medali ya dhahabu katika michezo ya
majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika(SARPCCO) inayoendelea nchini
Swaziland.(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi-Swaziland)
Na. Frank Geofray-Jeshi la
Polisi,Swaziland.
Mwanariadha
wa Polisi Tanzania, Basil John amefanikiwa kupata medali mbili za dhahabu baada
ya kushika nafasi ya kwanza katika mbio za mita 1500 na mita 800 katika Michezo
ya tisa ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) inayoendelea
katika mji wa Mbabane Swaziland.
Mwanariadha
huyo aliweza kuwashinda wanariadha wenzake baada ya kutumia dakika 1:49:00
katika mbio za mita 800 na katika mbio za mita 1500 aliweza kutumia dakika
3:49:02 na kuwaacha kwa mbali wanariadha kutoka nchi ya Zimbabwe na Swaziland
ambao walionyesha ushindani mkubwa.
Mwanariadha
mwingine kutoka Tanzania aliyeweza kupata medali ya dhahabu ni Fabian Nelson katika
mbio za mita 5000, ambapo aliweza kutumia dakika 14:27:33 na hivyo kuifanya
bendera ya Tanzania kupepea vyema katika michezo hiyo.
Ushindani
mkubwa katika riadha upo kati ya Zimbabwe, Tanzania, Namibia na Swaziland
ambapo nchi ya Swaziland imekuwa ikifanya vizuri katika mbio fupi.
Katika
Michezo ya Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na Wanariadha kumi na mbili ambapo
mpaka sasa tayari wameshafanikiwa kuchukua medali 4 za dhahabu, mbili za fedha
na moja ya shaba.
MTANZANIA ASHINDA MEDALI MBILI ZA DHAHABU SWAZILAND.
Reviewed by crispaseve
on
07:50
Rating:
Post a Comment